Infantino kushuhudia Simba, Al Ahly

DSM: RAIS wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA), Gianni Infantino atakuwa uwanja wa Benjamini Mkapa kushuhudia mchezo wa mashindano ya African Football League Simba SC dhidi ya Al Alhy utakaochezwa Oktoba 20 uwanjani hapo.
Taarifa ya ujio wa kiongozi huyo imetolewa leo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Iman Kajula, ambapo ameongeza kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe pia atakuwepo na marais wa vyama vya soka vya maeneo mengine.
Kajula amezungumzia ukarabati wa uwanja wa Mkapa kwa kuishukuru serikali kwa ukarabati huo ambao kufikia Oktoba 9, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro alisema ukarabati umefikia asilimia 95.
“Tunaishukuru serikali kwa matengezo makubwa ambayo imefanya kwenye uwanja wa Mkapa. Simba pia imetoa mchango kiasi kufanikisha hili.
“amesema Imani Kajula.