BEKI wa Simba SC, Henock Inonga ameacha maswali kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo baada ya kuweka alama za ‘emoji’kwenye’ instagram story’ yake zinazoashiri mtu anayetoa machozi na kuaga.
Alama hizo hazijaambatana na maneno yoyote kama mlinzi huyo anaondoka au kuna namna nyingine amemaanisha.
Baada ya kumalizika kwa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 zilianza tetesi kuwa huenda beki huyo asisalie Simba huku ripoti zikieleza klabu ya Far Rabat ya Morocco inamhitaji.
Inonga ni miongoni mwa mabeki walioonesha uwezo mzuri kwenye michuano ya AFCON ambapo aliisaidia timu yake ya DR Congo kufika nusu fainali.
Desemba 25, 2022 uongozi wa Simba ulimuongezea mkataba wa miaka miwili Inonga. Mkataba huo utamalizika 2025 hivyo baada ya msimu huu kuisha atakuwa amebakisha mwaka mmoja.