Inonga mgeni rasmi Simba vs Jwaneng
DAR ES SALAAM: MENEJA Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amemtaja mlinzi wa kati wa kikosi hicho, Henock Inonga Baka kuwa mgeni rasmi katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Jwaneng Galaxy kutoka Botswana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 26, Ahmed Ally amesema wamemchagua Inonga kumpa heshima kwa kuwa mshindi wa tatu wa michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) ililotamatika hivi karibuni nchini Ivory Coast.
“Tunampa heshima yake kwakuwa amefanya makubwa akiwa na taifa lake la Congo, na makubwa aliyoyafanya Inonga yanareflect Simba Sports Club kwa hiyo tunampa kuwa mgeni rasmi.” Amesema Ahmed Ally.
Mchezo huo wa maamuzi kwa miamba hiyo ya Kariakoo utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 02, 2024 saa 01:00 usiku na tayari kikosi hicho kipo kambini kujiandaa na mchezo huo.