IPA washauriwa kuongeza mafunzo kwa viongozi

KATIBU Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Ahmed Said, amelitaka Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA) kuongeza nguvu katika utoaji wa mafunzo mahsusi kwa viongozi na watumishi wa kada za juu ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na utoaji wa huduma za umma.

Akizungumza katika mahafali ya 18 ya chuo hicho yaliyofanyika Tunguu, Mhandisi Zena amesema IPA imekuwa ikitoa mafunzo ya muda mfupi yanayowalenga zaidi watumishi wa kada za chini na kati, huku kundi la viongozi waandamizi likikosa mafunzo maalum ya kuwaongezea ujuzi unaohitajika kwa majukumu yao makubwa ya kiuongozi.

Amesema ipo haja kwa chuo kuelekeza nguvu kuwafikia viongozi kulingana na mahitaji yao ya mafunzo na muda wa upatikanaji, hatua itakayosaidia kuimarisha mifumo ya uongozi, kuongeza uwajibikaji na kuboresha huduma kwa jamii.

Mhandisi Zena amehakikisha kuwa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora (KSUUB), ipo tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha viongozi wanashiriki ipasavyo katika mafunzo hayo. “Tunahitaji uongozi imara, wenye weledi na unaojibu mahitaji ya taifa. Tuko tayari kutoa kila aina ya ushirikiano,” alisema.

Awali, akisoma risala ya chuo, Mkuu wa IPA, Dk. Shaaban Mwinchum Suleiman, alisema chuo kinaendelea kupanua wigo wa huduma kwa kuboresha ubora wa elimu na mafunzo ya uongozi, sambamba na kuanzisha programu mpya zinazohitajika na taifa.

Amesema kwa mara ya kwanza IPA imeanzisha Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Uongozi wa Rasilimali Watu (MSc in HRM), programu ya mwaka mmoja na nusu, yenye lengo la kuandaa viongozi na wataalamu wa kusimamia watu na mifumo ya utendaji. “Tunataka wahitimu wetu wawe nguzo ya mabadiliko katika sekta mbalimbali,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Mmanga Mjengo Mjawiri, alisema Baraza limeendelea kusisitiza umuhimu wa IPA kuimarisha mafunzo mafupi ili kuwafikia watumishi wengi zaidi, hatua inayoweza kuchochea mabadiliko ya haraka katika utumishi wa umma. “Mafunzo mafupi ni njia ya haraka ya kuongeza ujuzi wa watumishi na kuboresha huduma,” alisema. SOMA: Rais Mwinyi atunukiwa Shahada ya Heshima Zanzibar

Baadhi ya wahitimu walisema wako tayari kutekeleza maelekezo waliyopatiwa na viongozi, wakibainisha kuwa dhamira yao ni kuendeleza safari ya elimu na kujiboresha ili kuendana na mabadiliko ya dunia. Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 786 walitunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali, wakiwamo wanawake 474 na wanaume 312, katika programu za Astashahada, Stashahada na Shahada ya Kwanza.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button