Iramba wamshukuru Rais ruzuku ya mbolea

WAKULIMA wilayani Iramba mkoani Singida wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan,kwa kutoa ruzuku ya mbolea katika msimu huu wa kilimo ambayo wamekiri wameanza kuona matokeo ya ruzuku hiyo mashambani.

Hayo yamesemwa leo na wananchi wa Kata ya Ulemo wilayani hapa mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo akiendelea na ziara yake mkoani humo kukagua utekelwzaji wa ilani ya CCM mwaka 2020/25, kukagua uhai wa chama mashinani na kuzungumza na wananchi.

“Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa mbolea ya ruzuku,tumeona matokeo yake katika mashamba yetu,tumeona big result now (tumeona matokeo makubwa sasa)” amesema Peter Paulo mbele ya Chongolo.

Rais Samia Agosti mwaka jana akiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima mkoani Mbeya alizindua mpango wa utoaji ruzuku kwa wakulima na kusema katika msimu wa mwaka 2022/23 serikali imetoa shilingi bilioni 150 kusaidia bei ya mbolea kushuka.

Bei ya mbolea imepanda kwa miaka mitatu mfululizo katika soko la dunia kutokana na janga la corona,vita ya Urusi na Ukraine na athari za uchumi duniani hali iliyofanya mfuko mmoja wa mbolea kufika shilingi 145,000 kutoka shilingi 60,000.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button