Iran yanyonga wawili kwa kukufuru

Iran yanyonga wawili kwa kukufuru

Iran imewanyonga wanaume wawili waliopatikana na hatia ya “kuchoma Quran” na “kumtusi Mtume wa Uislamu,” imesema mahakama ya nchi hiyo.

Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli-Zare walikuwa wakiendesha akaunti nyingi za mitandao ya kijamii “zinazomkana Mungu na kukiuka maadili ya kidini “, liliripoti  Shirika la Habari la Mahakama la Mizan.

Wakili wa Mehdad alikuwa amesisitiza kwamba hakuwa na hatia na hukumu yake haikuwa ya haki.

Advertisement

Kikundi cha kutetea haki za binadamu kiliita kunyongwa kwao “kitendo cha kikatili cha utawala wa kale”.

Kumekuwa na wimbi la mauaji ya kunyonga katika Jamuhuri hiyo ya Kiislamu, huku ghasia za upinzani dhidi ya serikali zikiendelea, lakini mauaji hayo ni nadra kwa waliopatikana na hatia ya kukufuru.

Mizan ilisema Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli-Zare walinyongwa katika Gereza la Arak katikati mwa Iran Jumatatu asubuhi.

Wanaume hao wawili walikamatwa mwaka wa 2020 na kushutumiwa kwa kuendesha kituo cha Telegram kiitwacho “Ukosoaji wa Ushirikina na Dini”, kulingana na Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu la Iran (HRANA).