SERIKALI imeshauriwa kuisaidia Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN) ili waweze kulipwa madeni wanayozidai Taasisi za Serikali.
Ushauri huo umetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Bungeni jijini Dodoma leo Mei 19, 2023 wakati uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyeliti wa Kamati hiyo, Mjumbe wa Kamati Abubakar Asenga amesema kutokana na ununuzi wa mitambo inayoendelea kufanyika, serikali iendelee kuisimamia TSN ili waweze kujiendesha kibiashara na kamati inazishauri Taasisi za Serikali kutumia TSN katika huduma za machapisho, majarida na makala.
Amesema Sekta ya Habari na Mawasiliano ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwani sekta hii huwezesha sekta nyingine zote kuweza kufikia malengo