Israel yawajibu Hamas

ISRAEL inasema iko kwenye “vita” baada ya Hamas kutangaza kuanza kwa Operesheni Al-Aqsa Mafuriko.
Vyombo vya habari vya Israel vinasema watu sita wameuawa na karibu watu 200 wamejeruhiwa katika mashambulizi yanayoendelea ya Hamas, kwa mujibu wa taarifa kutoka hospitali mbalimbali.
Jeshi la Israel linasema limeanzisha “Operesheni ya Upanga wa Chuma” dhidi ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza, kujibu mashambulizi kutoka eneo hilo.
Wizara ya Afya ya Palestina imesema mtu mmoja ameuawa katika shambulizi la kulipiza kisasi la Israel lililoikumba Hospitali ya Indonesia Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Imeongeza kuwa watu kadhaa pia wamejeruhiwa.