Jaju awauma sikio watumishi wa hifadhi

MBOGWE: Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbogwe Jacob Julius amewataka watumishi wa hifadhi za Taifa na mapori ya akiba TANAPA na TFS kufanya kazi kwa uadilifu na kuzidisha mahusiano mema na jamii.

Jacob ameyasema hayo leo Novemba 7, 2023 katika kikao kazi na watumishi hao wilayani Mbogwe

Amesema, wanapaswa kushirikiana na jamii na si kuishi kama maadui.

Advertisement

“Toeni ushirikiano wa kutosha kwa jamii, timizeni wajibu adhimu wa kutunza maliasili za Taifa pamoja na misitu, “amesema Jaju

Amesema  kufanya kazi kwa uadilifu ndiko kutachochea jamii kutoa ushirikano hata pale ambapo baadhi ya watu wanafanya matendo haramu ndani ya hifadhi .

Wakati huo huo, Jacob ametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba ya waalimu pamoja na matundu ya vyoo katika shule ya Bunyihuna ambazo serikali imetoka Sh milioni 73 .

Aidha, amemuagiza Mwalimu Mkuu wa shule hiyo pamoja na kamati ya ujenzi kufanya vyovyote wawezavyo kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *