Jambazi sugu auawa akiwakimbia polisi Arusha

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Dangote anayedaiwa kuwa ni jambazi sugu aliyeua watu zaidi ya saba mkoani Arusha amekufa katika harakati za kutaka kuwatoroka polisi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka kwa raia wema na jeshi la polisi vilieleza kuwa Dangote alikamatwa majira ya saa 3 na saa 5 leo asubuhi katika maeneo ya Ngarenaro kata ya Unga LTD akiwa katika nyumba ya mmoja aliyokuwa akijificha baada ya kufanya matukio ya uhalifu.

Habari zilisema kuwa baada ya polisi kupewa taarifa ya kuwemo katika nyumba hiyo katika eneo hilo kutoka kwa raia wema ndipo mtego ulipowekwa na kufanikiwa kumkamata akiwa hai ndani ya nyumba hiyo.

Vyanzo vilisema baada ya kukamatwa polisi walimuhoji na kutaka kutaja kundi zima walilokuwa wakifanya nalo uhalifu wa kupora mali na vitu vyenye thamani na baada ya kupora kuuwa katika matukio mbalimbali jijini Arusha ndio alipomtaja mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Omari Mkazi wa kata ya Lemara jijini Arusha.

Imeelezwa Dangote aliomba kutoa ushirikiano kwa kumwonesha Omari mahali anapoishi na msafara wa kwenda Lemara ulipoanza lakini walipofika kata ya Themi karibu na kiwanda cha Bia TBL Dangote aliruka gari na kwa lengo la kuwakimbia polisi.

Vyanzo vilisema kuwa baada ya kutaka kufanya jaribio hilo la kuwatoroka polisi inadaiwa kuwa alianguka sehemu mbaya iliyopelekea kupasuka kichwa na kufa hapo hapo na kutokwa na damu nyingi kwani gari la polisi lilikuwa katika mwendo mkali.

Habari zilisema baada ya Dangote kufa hapo hapo askari polisi walichukua mwili wake na kwenda kuhifadhi katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospital ya Mkoa ya Mount Meru kwa hatua zaidi za kiuchunguzi.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha,Justin Masejo hakuweza kupatikana kueleza tukio hilo kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa haipatikani mara zote.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
18 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Lorrainemith
Lorrainemith
17 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 17 days ago by Lorrainemith
Join
Join
16 days ago

Vyanzo vilisema kuwa baada ya kutakagwa kufanya jaribio hilo la kuwatoroka polisi inadaiwa kuwa alianguka sehemu mbaya iliyopelekea kupasuka kichwa na kufa hapo hapo na kutokwa na damu nyingi kwani gari la polisi lilikuwa katika mwendo mkali.

Sema alipigwa risasi ya kichwa

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x