James aweka rekodi, afunga pointi 39,000
MTAALAM wa mpira wa Kikapu LeBron James amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga pointi 39,000 kwenye NBA wakati LA Lakers wakiwashinda Utah Jazz katika mashindano ya ndani ya msimu.
Akihitaji pointi tano, alifunga 17 katika ushindi wa 131-99 mjini Los Angeles ambao walijihakikishia nafasi ya robo fainali.
–
James, 38, alimpita gwiji wa Lakers, Kareem Abdul-Jabbar aliyefikisha pointi 38,387 mwezi Februari na kuwa mfungaji bora wa muda wote.
–
“Kumekuwa na wachezaji wengi wazuri kwenye ligi hii tangu mwanzo wa wakati, na wafungaji wengi wazuri”
“Kuwa na uwezo wa kuwa wa kwanza wa kitu chochote daima ni kizuri kwa hakika.” Amesema LeBron
–
James ni mchezaji wa thamani zaidi ( MVP ) wa NBA mara nne.