Jamii ipatiwe elimu sahihi kutokomeza malaria 2030

MWENYEKTI wa Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania,  Leodegar Tenga amewataka wajumbe wa baraza  hilo kuwa karibu na wadau wa maendeleo ya afya ili kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030.

Tenga ametoa agizo hilo leo Juni 28, 2023  wakati  Baraza hilo lilipotembelea kiwanda cha Viuadudu Kibaha mkoani Pwani na kujionea shughuli zinazofanyika katika kiwanda hicho.

Tenga amesema ili kufanikisha kutokomeza malaria nchini jamii inapaswa ipatiwe elimu sahihi ya matumizi ya afua mbalimbali ikiwemo matumizi ya viuwadudu katika kuharibu mazalia ya mbu katika mazingira.

Advertisement

Aidha, Tenga ametoa Rai kwa Serikali kuhakikisha halmashauri zote nchini hususani zenye kiwango kikubwa cha Malaria kununua na kutumia viwadudu vinavyotengenezwa katika kiwanda cha Tanzania Biotech Product Limited.

Kwa upande wa mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo, Faraja Kotta, amesema kuwa ziara hiyo imekuwa chachu kwao kwani amejifunza na kuona nafasi ya dawa katika vita vya kutokomeza malaria nchini.

Amesema, dawa zinatengenezwa hapa nchini  zinaweza kutumika kuharibu mazalia ya mbu na kufanya Tanzania kuwa salama juu ya malaria kwa kuua mazalia ya mbu kabla hajasambaza vimelea kwa mtu.

“Tumepata chachu ya kubuni mikakati itakayo saidia kujibu changamoto za sehemu husika katika vita dhidi ya malaria Tanzania ambapo tunaona maeneo yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya malaria afua zake haziwezi kuwa sawa na maeneo yaliyonakiwango cha chini.|” Amesema

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *