Jamii ishirikishwe vita dawa za kulevya

Mkuu wa Mkoa Tanga, Omar Mgumba, akizungumza na Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii nchini, Faustine Shilogile.

JESHI la Polisi nchini limeshauriwa kuishirikisha jamii katika  mapambano ya kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya, biashara za magendo na wahamiaji haramu.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba, wakati akizungumza na Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii nchini, Faustine Shilogile, ambaye yupo mkoani Tanga, kwa ziara ya kuhamasisha jamii kushirikiana na kudhibiti uhalifu.

Amesema bila ya kuishirikisha jamii kwa ukamilifu, hizo changamoto haziwezi kumalizika, hivyo kusababisha madhara zaidi kwa watu ikiwemo na serikali kwa ujumla.

Advertisement

“Kila penye changamoto kuna fursa inajitokeza, hivyo licha ya mkakati wa mkoa kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa amani na uhalifu, lakini ni vizuri polisi mkatoa elimu kwa jamii umuhimu wa kusaidia vyombo vya usalama katika mapambano hayo,”amesema RC Mgumba

Naye Kamishna Shilogile amesema: “Tunajua jeshi la polisi hatuwezi kutosha pekee yetu kupambana na uhalifu katika maeneo mbalimbali, hivyo nimekuja kuhamasisha ushirikiano na jamii kuimarisha usalama wa nchi yetu na mipaka yake.”