Jamii yashauriwa namna ya kupunguza magonjwa sugu

KATIKA kuunga mkono jitihada za Wizara ya Afya za kupunguza magonjwa sugu, jamii imeshauri kutumia virutubisho mbalimbali ili kuondokana na changamoto hiyo.

November 9, 2021 serikali ilikamilisha mapitio na kupata rasimu ya mwisho ya Mkakati wa Taifa wa Afya Moja itakayotumika kati ya mwaka 2020 hadi 2026, wenye lengo la kupambana magonjwa sugu.

Akizungumza na Mtandao wa HabariLEO, Mkurugenzi wa Kampuni ya Elvin Agri, Darpan Pindolea alisema baadhi ya virutubisho vya kuondokana na changamoto ya magonjwa mbalimbali vinapatikana katika kampuni hiyo.

Alitaja baadhi ya magonjwa sugu yenye ufumbuzi wa virutubisho hivyo kuwa ni, kansa, magojwa ya uzazi, presha na kisukari na kuongeza kuwa virutubisho vimedhibitishwa na Shirika la Viwango (TBS).

Aidha, Pindolea ameshauri elimu itolewe kwa watanzania namna kutumia virutubisho hivyo, ambapo alisema kuwa wenye uhitaji wanaweza kufika Wilaya ya Bagamoyo kupata ufumbuzi zaidi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x