Jamii yatahadharishwa upandaji maua kiholela

MSIMAMIZI wa kituo cha Taifa cha kudhibiti matukio ya Sumu (NPCC) iliyopo katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) Yohana Goshashy ametahadharisha jamii kuacha kupanda maua majumbani kiholela badala wake wawaone wataalamu ili aweze kuwaonesha maua ambayo hayana madhara.

Wakati wa mahojiano maalum na HabariLEO, Goshashy alisema yapo baadhi ya maua ambayo yanasumu ambazo zinaweza kusababisha madhara ikiwemo kifo.

Amesema sumu ya baadhi ya mimea yanaweza kusababisha mzio kwa watoto hasa wakigusisha na sehemu kama macho na mdomo wanaweza kuwashwa macho na midomo kuvimba, wengine kulazwa hospital na wengine kupoteza maisha endapo wakitafuna mbegu za maua husika.

Advertisement

“Maua yanapokuwa karibu na nyumba au kupandwa ni vyema wakajua tabia husika ya maua wakati wanapopanda na waone umuhimu wa kuangalia watoto wakati wa kucheza wasije kukumbana na matukio ya sumu kwasababu baadhi ya maua yanasumu.

Ameongeza “Kila anayepanda maua nyumbani ahakikishe ni salama kuna watu wanajua mambo ya maua na miti lakini hata wakitupigia tunaweza kumwonesha maua hatarishi na kuchukua tahadhari.

Amesema miongoni mwa maua ambayo yanaweza kysababisha madhara yanajulikana kwa jina la Mnyonyo ambao unasumu inayoweza kusababisha kifo.

“Maua hayo mengi yanamajina ya kisayansi lakini kuna mmea wa kawaida ambao wengine wanatumi kwa tiba pia na urembo yanaitwa mnyonyo yanasumu ambayo yanaweza kupelekea kifo.

” Cha msingi ni mtu kujua aina ya maua ambayo anayo nyumbani kwakwe kuna yenye sumu ila ukiwa na ufahamu utachukua tahadhari kuna mengine yanafanana na Mkonge huwa yanasumu pia,”amesisitiza.

Amewashauri jamii kuwa ni vyema kupanda mboga badala ya maua ili kupata chakula.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *