Jamii yatakiwa kulea watoto kwenye maadili

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima amezitaka jamii kutekeleza jukumu la kulea watoto katika maadili ili kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili.

Dk Gwajima ameyasema hayo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa 12 Bunge, jijini Dodoma Aprili 14, 2023.

“Hivi karibuni Taasisi hii imeyumba, familia zimekuwa “busy” kufuatilia mali kuliko malezi ya familia wakati chimbuko la vitendo vyote vya ukatili ni familia kutoka kwa ndugu, jamaa” amesema Waziri Dk Gwajima

Dk Gwajima pia amebainisha jitihada zinazofanywa na serikali za kulinda maadili na Ustawi wa Jamii ikiwemo juhudi mahususi za Rais Samia Suluhu za kuanzisha wizara na kuundwa kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii.

Aidha amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ambao unaboreshwa zaidi ili kuendana na wakati na kutatua changamoto zinazojitokeza katika jamii.

Habari Zifananazo

Back to top button