Jamii yatakiwa kulea yatima

JAMII imetakiwa kuacha kutumia yatima kujipatia faida, badala yake waone kuwa jukumu la kulea yatima ni la wote.

Akizungumza na Habari Leo, Maria Msaada ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sauti ya Yatima Tanzania ametaja kuwa tabia ya baadhi ya watu kutumia yatima kwa faida zao binafsi ni changamoto inayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya yatima nchini.

Mkurugenzi huyo amesema kuna haja ya jamii kuunganisha nguvu ya pamoja ili kuwasaidia yatima kufikia malengo yao.

Advertisement

“Sababu ya kuanzisha kituo hiki cha kusaidia yatima ni kwa sababu mimi ni mmoja wa watoto waliolelewa katika vituo vya Yatima Tanzania.

“amesema Maria

Katibu wa Taasisi hiyo, Frank Mbwana, amedokeza malengo ya taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha maisha ya watoto yatima yapo salama na kuyaboresha katika nyanja zote.

“Ombi kwa Mkuu wa majeshi Tanzania kuwasaidia katika baadhi ya changamoto ambazo ni uhaba wa chakula, vifaa vya shule na uboreshaji wa mazingira ya watoto.” amesema Mbwana

Kwaniaba ya Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Tanzania, JKT Kamanda wa kikosi Mgulani JKT, Luteni Kanali Antony Ernest Sambila, amewataka viongozi wa Sauti ya Yatima kutokata tamaa, huku akidokeza kuwa JKT imeunga mkono Taasisi hiyo kwa matoleo yenye thamani ya milioni 4.

Taasisi ya Sauti ya Yatima imeanza mwaka 2006 na hadi sasa ina zaidi ya watoto yatima 200 inaomba msaada kwa mtanzania yoyote anayeguswa na watoto wenye uhitaji.