Jamii yenye uhitaji yakumbukwa

PWANI:Taasisi isiyo ya kiserikali ya Forester Nation Tanzania imetoa msaada zaidi ya Sh milioni saba kwa kununua mahitaji muhimu kwenye kituo cha kulelea watoto wenye uhitaji cha Ermanet Glory Home (PGH) kilichopo mkoani Pwani lengo likiwa ni kuwapa faraja.

Akizungumza leo  Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Amani Mbise, amesema wanatoa misaada hiyo kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wanachama wao ili kusaidia jamii yenye uhitaji.

Mlezi wa kituo hicho, Days Sylivester ameishuruku taasisi hiyo na kusema wanakabiliwa na changamoto ya vyumba vya kulala kwa watoto wa kiume pamoja na bima ya afya.

Nae Mdau wa Forester Nation Tanzania kutoka kampuni ya Chrysos Crop limited ya Australia Ernest Kihampa aliyeshiriki amesema wanaweka kipaumbele kwa kuisaidia jamii iliyosahaulika.

 

Habari Zifananazo

Back to top button