“Jamii zinufaike uwekezaji madini”

DAR ES SALAAM: KAMPUNI za madini nchini zimetakiwa kuboresha huduma za jamii kwenye vijiji vinavyozunguka migodi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama vile barabara, maji, vituo vya afya na shule.

Hiyo ni sehemu ya mikakati ya utekelezaji wa Dira ya Madini ya 2030 iliyoainishwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba leo jijini Dar es Salaam ambapo imejipambanua kwa moto wa ‘Madini ni Maisha na Utajiri’.

Mhandisi Samamba amesema Tume ya Madini imejipanga kuboresha usimamizi wa Sekta ya Madini. Katika kutekeleza hayo imejikita katika kuwainua wachimbaji wadogo nchini kwa kuendelea kutenga maeneo yaliyofanyiwa utafiti wa kijiolojia kwa wachimbaji wadogo ili uchimbaji wao uweze kuwa na tija pamoja na kuhakikisha kipaumbele kinatolewa kwa watanzania kwenye utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini nchini.

Amesema kuwa utekelezaji wa Dira hii katika Sekta ya Madini inawalenga zaidi wachimbaji wadogo wa madini ambao wamekuwa wakiwekeza lakini manufaa yamekuwa si ya kuridhisha kutokana na kutokuwa na taarifa za kutosha za utafiti za madini na teknolojia duni kwenye uchimbaji wa madini.

Amefafanua kuwa Tume itaendelea kuimarisha usimamizi katika shughuli za madini kwa kutenga maeneo yenye taarifa za kijiolojia yaliyofanyiwa tafiti ili kuweza kunufaika na rasilimali hizo sambamba na kuandaa Mpango Kazi utakaolenga kusimamia maeneo ya elimu za ugani; kuboresha mfumo wa utoaji wa leseni; ukaguzi migodi na mazingira; usimamizi wa masuala ya afya na usalama mahala pa kazi pamoja na kuimarisha mifumo ya makusanyo ya maduhuli.

Mhandisi Samamba amesema katika kutekeleza dira ya madini ya 2030, Tume imejikita katika kutoa elimu kwa wamiliki wote wa migodi kuhusu kutoa kipaumbele kwa huduma na bidhaa zote zinazotolewa na watanzania pamoja na kuandaa namna bora ya kuingia ubia kati ya kampuni za watanzania na kampuni za nje na uwepo  wa utekelezaji wa Sheria ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini  pamoja na Urejeshaji wa Huduma kwa Jamii.

Ameendelea kufafanua mikakati mingine  kuwa ni pamoja na uwepo wa mfumo wa usimamizi wa ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini na kutoa elimu kwa wakandarasi wote ili kuwaandaa kushiriki katika mikataba yenye thamani kubwa kwa lengo la kuchangia ajira na kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini.

Tume ya Madini ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya Madini ambayo iliundwa kutokana na Sheria ya Madini Sura ya 123 na ilianza utekelezaji wa majukumu yake Mwezi Aprili, 2018 kwa kutekeleza majukumu 22, ambapo jukumu kubwa ni kusimamia na kudhibiti Sekta ya Madini nchini.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NAMONGO FC
NAMONGO FC
28 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)..

336385342_23852687669090184_4327056666681808736_n-1699524871.7938-300x300.jpeg
AlmaRankin
AlmaRankin
Reply to  NAMONGO FC
28 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website________ http://Www.Careers12.com

Last edited 28 days ago by AlmaRankin
NAMONGO FC
NAMONGO FC
28 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)..

400691249_864990868631687_149643332150728266_n-1699514610.2614-1699523863.3682-212x300.jpg
NAMONGO FC
NAMONGO FC
28 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI).

400652614_122123967464061853_6811123058608430011_n-1699514588.5978-200x300-1699523844.9688.jpg
NAMONGO FC
NAMONGO FC
28 days ago

IKIFIKA WALIOPO HAWATOSHI… WATANZANIA 3 WANATAFUTWA… 1. MKULIMA MKUBWA (TAASISI ZA SERIKALI) 2. MKULIMA WA KATI (MWEKEZAJI MKUBWA SANA) 3. MKULIMA MDOGO (ANAYELIMA NYUMBANI)….

396913935_270519422649565_3279129179102033513_n-1699514567.7649-232x300-1699523827.9501.jpg
NAMONGO FC
NAMONGO FC
28 days ago

USALAMA KAZI MHE TUTAFANYA KWA AJILI YA “MLIMA KILIMAJARO” – LAZIMA TUFANYE KITU KWA AJILI YA TANZANIA USALAMA WETU TUKITEMBELE

OSK-1699526502.5327-300x200.jpeg
trackback
28 days ago

[…] post “Jamii zinufaike uwekezaji madini” first appeared on […]

Angila
Angila
28 days ago

I get paid over $87 per hour working from home with (Qk)2 kids at home. I never thought I’d be able to do it but my best friend earns over 10k a month doing this and she convinced me to try. The potential with this is endless. 
.
.
.
.
Here’s what I’ve been doing…> > > http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
8
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x