BALOZI wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza bunifu na ujasiriamali kwa njia ya kidigitali ili kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Akizungumza leo katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)wakati wa kusikiliza mawasilisho ya program ya next Innovation with Japan(NINJA) Misawa amesema Japan International Cooperation Agency (JICA) inaunga mkono wabunifu vijana na wajasiriamali wa Tanzania.
“Japan pia imeendelea kiteknolojia tuna uzoefu na ukuaji wa haraka hivyo tunahitaji kushirikiana na vijana wa kitanzania kuleta utatuzi wa changamoto zilizopo,”ameeleza.
Amesema washiriki katika mradi wa NINJA wamewasilisha mafanikio yao ambao wamekuza biashara mpya na kuanzisha kampuni na zimefanikiwa ndani na nje ya nchi na ambayo imewezeshwa na JICA.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Makamu wa Chuo kikuu cha Dar es Slaam anayeshughulika na masuala ya utafiti ,Prof Nelson Boniface amebainisha kuwa JICA na Ubalozi wa Japan unaleta vijana katika masuala ya biashara na leo (jana) wamefanya mawasilisho mbalimbali katika makundi mawili .
“La kwanza linaonesha akinamama ambayo wamekuwa na mawazo ya kibishara na wameshakuwa na bidhaa ambayo inaitwa ‘Mrembo natural product’ ambayo ilianza baada ya tatizo la kutumia kemikali za kutengeneza nywele akapata madhara akaamua kutafuta mbadala kwa kutumia matunda asilia kutunza nywele.
Amesema kundi la pili inatumia program tumizi (application) ambayo anatumia kushauri vijana na wanawake kuwa na tabia ya kutunza mali zao kwa maana ya fedha na matumizi na wameshaanza kufanya kazi.
Aidha amesema changamoto zinazowakumba ni uzalishaji akitolea mfano wa Mrembo Natural product ambapo uzalishaji ni mdogo na uhitaji ni mkubwa.
“Tunawale vijana na jinsi ya kuendeleza mawazo yao na kufanya kuwa biashara na kutatua matatizo ya kijamii kupitia mradi huu UDSM inafanya tafi ,kutoa huduma kwa jamii na tatu kufanya mambo ya ubunifu wa kutatua changamoto za jamii na tunafanya tafiti kubaini changamoto ili kupatia ufumbuzi ambao tunauita ubunifu.
Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania,Hitoshi Ara amesema wanaona uwezeshaji wa wanawake umepewa nafasi kubwa na wanaungana na serikali kuanzisha miradi mbalimbali na mwaka huu wanampango wa mradi wa wanawake ambao ni muhimu kuonesha matokeo mazuri na kazi nzuri.
Amefafanua kuwa pia wanalenga kuwawezesha vijana kwani pia nchi inawapa kipaumbele na wakati wanapozungumza kuhusu ukuaji wa kiuchumi kizazi cha vijana lazima kitajwe katika utumiaji wa rasilimali na kushiriki katika uzalishaji.
“Hivyo tunaangalia zaidi wanawake na vijana hasa kwa suala la ujasiriamali na uvumbuzi tunafanay mradi wa Ninja ili kufanikisha hilo,”amesisitiza.