Jata yawakumbuka wafungwa waliomaliza muda

UMOJA wa Watanzania waliosoma nchi mbalimbali (JATA ) umeweka mpango mkakati wa jinsi ya kuwafikia waliotoka gerazani kwa kuwajengea uwezo wa kuishi kwa kufanya miradi ya maendeleo itakayowapatia kipato.

Mwenyekiti wa JATA, Gregory Mlay alisema hayo wakati wa kikao kazi cha wanachama wake kilichofanyika mjini Morogoro kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA ).

Alisema kupitia kikao kazi hicho baina ya Viongozi wa Taifa (EXCOM) na Viongozi wa kanda za JATA , kilijadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya mwaka 2023/ 2024 na kuimarisha umoja huo .

Mlay alisema viongozi walioshiriki kikao kazi hicho ni kutoka Kanda ya Morogoro, Pwani, Kaskazini , Kusini, Iringa , Kanda ya Ziwa, Kati na Kanda ya Zanzibar .

Alisema miongoni mwa utekelezaji unakaofanyika kwa mwaka huu ni mradi jinsi ya kuwafikia waliotoka gerezani hususani Zanzibar ili kuwajengea uwezo wa kuishi kwa kufanya miradi itakayowapatia kipato .

Mlay alitaja hatua nyingine ni pamoja na jinsi ya kufuatilia na kuwafikia wanachama wa umoja huo waliopo katika kila kanda.

“Kwa mwaka huu tunatekeleza miradi sita ambayo ilipitishwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka jana ( 2022) na miongoni ni mpango mkakati wa jinsi ya kuwafikia waliotoka gerazani kwa kuwajengea uwezo wa kuishi kwa kufanya miradi ya maendeleo “ alisema Mlay.

Katibu Msaidizi wa Umoja huo, Edina Ngelageza alisema licha ya miradi hiyo sita ipo mingine ambayo inatekelezwa na mwananchama mmoja mmoja waliohitimu taaluma tofauti ikiwemo sekta ya afya, maji, viwanda, mazingira, elimu na utawala bora.

Ngelageza alisema miradi inayotekelezwa na mnufaika mmoja imekuwa na tija kwenye jamii ukiwemo mradi wa usafi wa mazingira unaotekelezwa kwenye halmashauri ya wilaya ya Iringa na kuifanyaiongoze kwa utunzaji mazingira nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa JICA , Evona Mathew alisema shirika hilo linajivunia kwa kiasi kukibwa uundaji wa umoja wa watu waliosoma Japan chini ya ufadhili wa shilika lao.

“ Hii imekuwa ni njia sahihi ya kufatilia na kubaini matunda ya ufadhili wa JICA unaoutoa katika sekta mbalimbali kwani unaleta tija katika jamii” alisema Evona.

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button