Je, ni hatari kuogelea baada ya kula?

Je, ni hatari kuogelea baada ya kula?

KILA majira ya joto, katika saa zinazoambatana na wakati wa chakula, kuna watoto kwenye ukwe au kando ya bwawa, wakingojea kwa subira mchakato mmeng’enyo wa chakula ukamilike.

Ni muda gani utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula hukamilika – Wataalamu wanasema huchukua kati ya dakika 30 na saa mbili – lakini inategemea na aina na wingi wa chakula.

Nini kitatokea ikiwa wataamua kupiga mbizi kabla ya wakati? Kitaalamu tukio hili linaitwa ‘digestive failure’ ambayo ni kushindwa kwa mmeng’enyo wa chakula.

Advertisement

Imani iliyopo ni kwamba ikiwa mmeng’enyo wa chakula haujakamili, mpiga mbizi anaweza kuzama.

Wazo la kwamba watu wanapaswa kusubiri kwa muda baada ya kula kabla ya kuogelea ni la kawaida katika nchi nyingi, lakini maelezo maarufu kuhusu kwa nini hutofautiana na uwezekano wa kushindwa kwa utumbo. 

Wataalamu wengine wanaonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuteseka na tumbo, ambayo inaweza kuwa hatari wakati akiwa majini. Wengine wanasema kuwa, kwa kuwa karibu damu yote ya mtu huelekezwa katika mmeng’enyo wa chakula, ni sehemu ndogo hufikia misuli ya mikono na miguu, na kumfanya mtu kushindwa kuogelea.

Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kisayansi unaounga mkono nadharia hizi. Kwa hivyo, kulingana na uchambuzi wa 2011 wa fasihi ya kisayansi inayopatikana juu ya mada hiyo iliyochapishwa katika Jarida la Kimataifa la Utafiti wa Majini na Elimu, “hakuna kesi zilizoripotiwa za kula kabla ya kuogelea na kusababisha au kuchangia kufa au kutokufa kwa kuzama majini.”

Msingi wa kisayansi wa utafiti huo unaendelea kusema kwamba “kula kabla ya kuogelea sio hatari inayochangia mtu kuzama na inaweza kutupiliwa mbali kuwa ni hadithi.” Walakini, watu bado wanazingatia ushauri huo.