Jela maisha kwa kosa la kunajisi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha imemhukumu kifungo cha maisha jela Shedrack Saitoti baada kukutwa na hatia ya kumnajisi mtoto wa miaka saba .

Akisoma hukumu hiyo leo, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo ,Kohawa Magreth Mboya amesema kuwa Saitoti amekutwa na hatia baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mimutie Women Organization Rose Njilo amesema kuwa wao kama taasisi ya kutetea haki za wanawake na watoto wameishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki kwani adhabu hiyo itarudisha maadili kwa jamii na kuwa fundisho kwa wengine.

Advertisement

Aidha Rose Njilo ameishukuru Women Fund Tanzania kwa kuendelea kuwa wezeshaji wa shirika la Mimutie katika kuibua changamoto za ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.

Wadau mbalimbali na wanaharakati walifika katika mahakama hiyo kusikiliza hukumu hiyo na kusema kwamba mahakama hiyo  imetenda haki kutenda haki kwa mshtakiwa kwani akusumbua mahakama kwamba akufanya tendo hilo la ulawiti kwa mtoto huyo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *