Jela miaka 2 kwa nyama ya pofu

RUVUMA: Tunduru. MAHAKAMA ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma  imemuhukumu  kifungo cha miaka miwili  jela   Ally Rashidi Mbalamla (30), Mkazi na Kijiji cha Muhuwesi Wilaya ya Tunduru, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za serikali.

Akisoma hukumu ya kesi ya Jinai Na.

7964 ya mwaka 2024, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Lilian Haule   amesema mahakama imefikia uamuzi huo, baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo kuacha shaka yoyote.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo  Desemba 01, 2023 kwa kukutwa na vipande 14 vya nyama ya pofu katika Kijiji cha Muhuwesi na kufikishwa mahakamani Machi 25, 2023 na siku hiyo hukumu kutolewa.

Habari Zifananazo

Back to top button