MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoani Katavi, imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela Majid Khalid Selemani (36) maarufu kwa jina la ‘Alsalimi’ mkazi wa Madukani Mpanda na Wahab Amory Said (29) mkazi wa Kawajense kwa kosa la kumnajisi mwanafunzi wa kidato cha pili.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Gway Sumaye, amesema licha ya kifungo jela, watamlipa muathirika wa tukio hilo Sh miliomi mbili kila mmoja.
Amesema vijana hao walitenda uhalifu huo kwa kumlawiti mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 15, tukio walilotekeleza kati ya Machi 1, 2022 na Machi 1, 2023.
Comments are closed.