Jenerali Fatuma kuongoza Jeshi la Anga Kenya
NAIROBI, Kenya: RAIS wa Kenya, William Rutto amemteua Jenerali Charles Kahariri kuwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi nchini humo kuziba nafasi iliyokuwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo, Francis Ogolla.
Kwa upande mwingine, Meja Jenerali Fatuma Ahmed ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Jeshi la Anga, ndani ya Majeshi ya Ulinzi ya Kenya (KDF).
Uteuzi huo wa kihistoria umetangazwa na Idara ya Ulinzi baada ya Rais Ruto kuidhinisha uteuzi wake.
Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed ameingia katika jeshi la Kenya mnamo 1984 na anakuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika historia ya jeshi hilo