Jengo mama na mtoto kujengwa hospitali ya rufaa Shinyanga

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Grace Magembe amesema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wanajenga jengo la mama na mtoto la gorofa tatu na maabara ambayo itakuwa imejitosheleza katika vipimo vya magonjwa mbalimbali kuwa sehemu moja.

Mhandisi mshauri na mjenzi amepatikana na leo amekuja rasmi kuanza vipimo kwaajili ya ujenzi wa majengo hayo ambapo itajengwa stoo ya kuhifadhi dawa (famasi) mochwari na jengo la kufulia.

Dk Magembe amesema hayo leo katika ziara yake ya siku moja mkoani Shinyanga alipokuwa akikagua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, kituo cha afya Kambarage kukagua wodi ya wazazi na hospitali ya rufaa ya mkoa.

Dk Magembe amesema serikali imekwisha saini mkataba na mshauri mjenzi kuhusu ujenzi huo na eneo tayari uongozi wa hospitali ya rufaa umelionyesha kinachosubiri utekelezaji.

‘Hospitali hivi sasa zimepiga hatua kuwa na vifaa tiba vya kisasa kwani tumeona kuna mashine ya Tscan ambayo inafanya kazi na wananchi wanapata huduma karibu kuna majengo ya wagonjwa wa dharura ambayo yanavifaa.

“Kuna mtambo wa kuzalisha hewa ya gesi ambayo inasaidia kuwapa huduma hospitali zilizopo halmashauri za mkoa huu na mikoa ya jirani na mtungi mmoja uliojazwa hospitali hii wanaiuza kwa shilingi 10,000.”amesema Dk Magembe.

Dk Magembe amesema serikali imeweza kujenga vituo vya kuzalisha gesi hiyo kwenye vituo 24 nchini na mkoa wa Shinyanga ni mmojawapo ambapo zamani kabla ya kutokuwepo gezi walikuwa wakifuta mkoani Mwanza kwa gharama ya Sh 50,000 hadi 80,000 mtungi mmoja.

Dk Magembe amesema Serikali imetoa fedha lakini mradi inakuwa ikisuasua inatakiwa iendane na mkataba ulivyo ili wananchi wapate huduma iliyokusudiwa na hatua zingine zianze hivyo aliomba uongozi wa serikali ya mkoa kusimamia miradi iishe kwa wakati.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk Yudas Ndungile amesema yapo majengo matano yanayotoa huduma ya dharura na wataalamu wamepewa elimu na vifaa stahiki vipo hivyo huduma za dharura zimeimarishwa isipokuwa Manispaa ya Kahama wanatarajia kujenga majengo hayo

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa DK John Luzila amefurahi kuanza kwa mkakati wa ujenzi wa majengo hayo baada ya kuona utekelezaji unaanza huku akisema watu 449 mpaka sasa wametumia mashine ya Tscan iliyopo hospitalini hapo.

Habari Zifananazo

Back to top button