Jeshi la Polisi latakiwa kutunza maadili

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo

MKUU wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita,  Sakina Mohamed amewataka watumishi wa Jeshi la Polisi  kutii na kufuata yale yote ambayo yanaimbwa kwenye wimbo wa maadili wa Jeshi hilo kwakuwa wimbo huo umejaa kila aina ya makanyo yanayopaswa kufuatwa.

Sakina ameyasema hayo leo Januari 23, 2024 katika kikao kazi na jeshi hilo ambapo ameliltaka kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na kuondoa mazingira ambayo yatafanya wananchi kuona kana kwamba Jeshi la Polisi ni onevu.

Pia amelitaka jeshi hilo kuwa tayari na kuendelea kupambana na uhalifu ili wilaya na raia waendelee kuwa salama.

Advertisement

Amesema katika mwaka huu wa uchaguzi ni muhimu zaidi chombo hicho kujiimarisha ili Mbogwe ivuke salama na kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa iwe tulivu.

Katika hatua nyingine, Sakina amewataka jeshi la polisi kuweka mahusiano mema na wananchi ili kurahisisha utendaji na upatikanaji wa taarifa kwa jeshi hilo.