Jesus aumia tena
KWA mara nyingine Arsenal imekutana na pigo, baada ya taarifa za kuumia mshambuliaji wao Gabriel Jesus.
Kocha klabu hiyo, Mikel Arteta amesema Jesus atakosekana kwa wiki kadhaa akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu.
Alikuwa na shida katika goti lake ambalo lilimsababishia maumivu kwa hivyo ilibidi tumuache, atakuwa nje kwa wiki chache”.amesema Arteta.
Hii ni mara ya pili kwa Jesus kuumia kifundo cha mguu, ikumbukwe aliwahi kuumia Kombe la Dunia akiwa na Brazil na kumfanya kukosa baadhi ya mechi za Arsenal msimu ulioisha.