Jifunze Kiswahili

We proceed with our topic today

Chenga: Je,nikusindikize? Sina kazi,nitafurahi kwenda nawe.

Tatu:Ukitaka twende, Naogopa kwenda peke yangu.

Chenga: Ni bahati kwangu kupata nafasi hii.

Tatu:Bahati gani? Mbona tunaonana Kila siku?

Chenga: Ndiyo, lakini Leo ni tofauti na siku nyingine

Tatu:Tofauti gani? Mimi naona sawa tu kama Jana na juzi na siku zote.

Chenga:Iko tofauti, nitakwambia Sasa hivi, twende tu.

Tatu:Haya, niambie basi,kitu gani hicho?Siri,au nini?

Chenga:Usiwe na haraka,nitakwambia tu,ngoja kidogo,

Tatu:Ningoje nini? Niambie tu,Niko hapa,sitakukimbia.

Chenga: Nilitaka kukwambia tangu siku nyingi,lakini sikuwa na nafasi.

Tatu:Mbona inazidi tu kuzunguka husemi chochote cha maana.

Chenga:Ni hivi,ningependa wewe na Mimi,tukisha kuwa wakubwa tuoane,inasemaje?Hupendi kuwa mke wangu wa maisha?

Tatu:Maneno Yako hayana maana,kama umekosa la kusema heri kunyamaza.

Chenga:Najua huwezi kukubali mara Moja,nenda ukafikiri pole pole.

Tatu:Sina Cha kufikiri,inafaa tuongee mambo mengine ,Unaona basi lile

Chenga:Twende upesi,tutachelewa,mabasi hapa ni shida sana siku hizi.

Zoezi

1.Tatu alikutana na nani alipokwenda sokoni?

2.Nani alisema ,”Tofauti gani?

3.Nani alisema ,”kitu gani hicho?

4.Nani alimsindikiza Tatu?

5.Nani alisema,”Maneno Yako hayana maana?

6.Je mabasi ni rahisi au ni shida kuyapata?

Habari Zifananazo

Back to top button