Jifunze Kiswahili

DUKANI

Tatu aliwaambia watoto wake waende dukani kunununa vitu.Chausiku alisema ,”Mama nitakwenda peke yangu dukani siogopi kitu”Mashaka alivyosikia vile alifurahi kwa sababu hakuitaka kwenda dukani ;Alitaka kucheza mpira ,Basi ,chausiku aliondoka mara Moja.

Alifika dukani akakuta watu wengi ,Aliuliza ,”je,mchele uko?”Mwenye duka alijibu,”Mchele uko ,dada;unataka kiasi Gani?”chausiku alijibu” ,nipe kilo tano.nipe pia na nusu kilo ya binzari ,robo kilo ya pilipili na kilo moja viazi,Nipe upesi mikimbie nyumbani.

Advertisement

Mama ananingojea nyumbani njiani kwa sababu usiku umeingia nami Niko peke yangu ,mwenye duka alisema ,”Haya ,dada chausiku,vitu vyako hivi hapa ,nipe shilingi kumi na thumni ,”Chausiku alisema ,”Sina shilingi kumi na thumni “,Ninazo shilingi tisa na thumni tu ,”Mwenye duka alisema ,”Haya SI kitu,nipe hizo hizo tu,”Chausiku alitoa fedha ,akachukua vitu vyake ,akaondoka mbio,Alifika nyumbani kabla giza halijazidi.

MANENO MUHIMU

Dukani;madukani,.                     In ,at the shop(s);shopping centre.

Bei;bei gani?                                Price;what is the price?

Viatu vimepanda bei,.                Prices have gone up.

Punguza bei                                Reduce the price

Ongeza bei,pandisha bei           increase the price,

Ndizi hizi bei gani?                     What is the price of these bananas?

Samaki Hawa bei gani?              How much are these fishes?

Samaki mmoja ni shilingi mbili, They are two shilings each.

Si ghali ,ndiyo bei Yao,.                They are so dear?

Si ghali,ndiyo bei Yao,.                  They are not dear,that’s the price

Haya ,nipe mbili,.                           Well,give me two.

Usiuze ghali namna hii,.                Don’t sell at such a high price.

Nisipo fanya hivyo.                         If I don’t do that I will get no

Sipati faida                                      profit

Zoezi

1.Chausiku alinunua nini dukani?

2.Nani alikwenda dukani?

3.Je chausiku alinunua binzari kilo ngapi?