JK akutana na TMK Wanaume

RAIS  Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na wasanii nguli wa Bongo Fleva wanaounda kundi la Wanaume TMK ofisini kwake Masaki jijini Dar es salaam leo April 12,2023.

JK kakutana na kuzungumza nao maswala mbalimbali ikiwemo ya tasnia ya sanaa.

Advertisement

Wasanii hao, Juma  Nature, Chegge Chigunda na Amani James Temba au ‘Mheshimiwa Temba’ wamefurahi sana kupata kile walichokiita baraka za Mzee JK wakiwa katika kukaribia kumalizia ‘project’ yao ya pamoja mpya ambayo haijatajwa.

Kama itakumbukwa wasanii hao ndio waliounda kundi la TMK Wanaume Family lililokuwa kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Kundi hilo lilianzishwa rasmi mnamo Septemba 16 2002 jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa albamu ya Juma Nature iitwayo “Ugali” na hadi sasa limejijengea umaarufu katika albamu zake mbili ilizotoa ambazo ni “Kutokea Kiumeni” na “Ndio Zetu”.

Wasanii wa kundi hilo kabla ya wengine kujiengua ni Juma Nature, KR, Doro, D Chief, Mh Temba, Mzimu, Luteni Karama, Chegge, Yp, Y Dash, na wengineo.

Baada ya kutengana kukawa na “TMK Wanaume Halisi” na Tmk Wanaume. TMK Wanaume likiongizwa na Mhe. Temba na Chegge wakati TMk Wanaume Halisi kiongozi akiwa Juma Nature na Inspector Haroun.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *