RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, amesema ni wajibu kwa wafanyabiashara nchini kuona maonesho ya Sabasaba 2023′ kuwa ni soko la bidhaa zao kwa kukutana na wateja wa kitaifa na kimataifa.
Ameyasema hayo leo Julai 6, 2023 katika ziara yake kujionea bidhaa na shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi na mashirika ya serikali na binafsi kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
“Mzalishaji yeyote anazalisha kwa ajili ya soko, maonesho haya yanatoa fursa ya soko,” amesema.
Amewasihi wafanyabiashara kwa kutolea mfano wa watengeneza batiki, sabuni na bidhaa nyingine kutumia maonesho haya kutangaza bidhaa zao pia kutengeneza mitandao wanapokutana na wafanyabiashara ndani na kimataifa.
“Wanapokuja wawekezaji wa nje na wawekezaji wetu wanapokutana hapo wanaingia kwenye makubaliano ambayo yanaibua business deal,” amesema.
Comments are closed.