TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) itafanya upasuaji kwa watu wazima 20 wenye tatizo la mishipa ya moyo kuziba mishipa mikubwa ya moyo iliyotanuka au kupasuka katika kambi maalum ya matibabu ya wiki moja.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema jumla ya wataalam 160 watapata ujuzi kutoka kwa wataalamu wa Taasisi ya CardioStart ya nchini Marekani kuanzia Mchi 12 hadi 17,2024.
“Tunategemea ndani ya hii wiki tufanya upasuaji kwa wagonjwa 15 hadi 20 kuanizia kesho lakini wataalamu wetu 160 watapata elimu na kuongeza ujuzi kutoka kwa hawa madaktari kutoka nje na watashiriki kuanzi nesi,fundi mitambo na madaktari bingwa.
Aidha amesema tayari kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki na kati JKCI imeweza kubadilisha vulvu ya moyo bila kupasua kifua ambapo hayo ni matokeo ya kazi za Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imefanya JKCI kuwa moja ya taasisi 10 bora ya matibabu ya moyo kwa Afrika.
Amesema wamenunua mtambo mkubwa ambao haupo Afrika Mashariki na Kati na umenunuliwa kwa Sh bilioni 7 ambaao pia umeongeza wigo wa tiba utalii.
“Tunapata watalii karibu nchi 20 ni jambo kubwa kwasababu tumenza kupata watalii kutoka Ujerumani ,Ufaransa,Italiy,Poland wamekuja kufanya utalii na wakipata matatizo ya moyo walikuwa wanarudi kwao sasa wanakuja moja kwa moja kwenye taasisi,”ameeleza Dk Kisenge.
Ameongeza “Zaidi ya mashirika 20 yanakuja kwenye taasisi yetu wanavutiwa na vifaa vilivyowekwa na rasilimali watu wanaona wakifanya huduma wagonjwa watapona wanatoka mataifa mbalimbali kwasababu ya Dk Samia na mapinduzi makubwa.”
Pia amefafanua kuwa Rais Samia alitoa fedha nyingi kuwekeza katika elimu kwenye vyuo vya ndani kama vile JKCI kuanzisha program kwa kushirikiana na Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambapo hivi sasa wamejiunga na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pia kwa kozi za upasuaji wa moyo,tundu dogo na nesi.
“MUHAS wanatoa kozi ya udaktari bingwa wa upasuaji wa moyo karibu Sh bilioni 9 zimetolewa kwa ajili ya mafunzo ya ndani na nje ya nchi Kuna wanafunzi wako nje ya nchi serikali inawalipia ada.
Dk Kisenge amesema kuwa Rais Samia ametoa fedha kwaajili ya kutanua wigo wa matibabu ya magonjwa ya moyo ambapo JKCI sasa inaenda kufungua matawi katika Hospitali ya Chato,Zanzibar,Mbeya na tayari wanafunzi kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa wanafanya mafunzo kwani vifaa vimeshanunuliwa na huku Hospitali ya Kanda ya Rufaa (KCMC) wanaaza kujenga jengo la magonjwa ya moyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa upasuaji JKCI ,Dk Angela Muhiozya amesema wataalamu hao kuja hapo kumekuwa na manufaa makubwa na mabadiliko katika taasisi hizo kwani mbinu walizofundishwa mwaka jana zimeleta matokeo.