JKCI yaokoa zaidi ya sh bilioni 3 za matibabu nje ya nchi

DAR ES SALAAM Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imesema imeokoa zaidi ya sh.bilion tatu baada ya kambi ya  wataalamu wa moyo kutoka Saudi Arabia kufika katika Taasisi hiyo na  kutibu magonjwa ya moyo .

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dk.Peter Kisenge  amesema hayo leo Dar es Salaam wakati wa kuaga wataalamu hao wa Saud Arabia ambao wamekuwa nchini kwa siku saba kuanzia Septemba 9 hadi 15.

Amesema timu  kutoka Saudi Arabia wamekuwa wakifika nchini kuanzia mwaka 2015 na kutoa huduma mbalimbali za upasuaji wa moyo lakini pia kufundisha wataalamu wa moyo katika Taasisi hiyo ambapo fedha ambazo wamekuwa wakizitoa tangu walipoanza kufika Tanzania ni sawa na sh bilioni 3.5 na ambazo zimekuwa zikitumika kwa kutoalea huduma mbalimbali.

Advertisement

Amesema kwa kipindi chote ambacho wamekuwa wakifika nchini kupitia taasisi ya  kujitolea ya King Salman Humantarian , wamekuwa  msaada mkubwa  nchini  kwani kwa kipindi chote wamesaidia kutibu wagonjwa wa moyo zaidi ya 439.

Akielezea hali ya magonjwa ya moyo kwa watoto nchini, Dk.Kisenge amesema tatizo hilo ni kubwa duniani kwani Takwimu zinaeleza kuwa, kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa mmoja anatatizo la moyo, hivyo jitihada zaidi za matibabu zinahitajika Kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo vingi.

Kwa upande wake  Balozi wa Saud Arabia Nchini, Yahya Ahmed Okeish amesema  program ya kuhuduma watu imekuwa ikifanyika duniani kote kwa kuwa ni jambo la faraja kuona watu wakifurahi baada ya kupata huduma.

 

 

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *