IVORY COAST: Timu ya Jkt Queens leo itacheza mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFWCL) dhidi ya Sporting Club Casablanca ya Morroco.
Mpaka sasa mabingwa hao wa ukanda wa CECAFA wana alama tatu katika michezo miwili waliyocheza huko nchini Ivory Coast hivyo wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Kocha wa timu hiyo, Esta Chaburuma amesema wanazihitaji mno alama tatu za mchezo huo licha ya kwamba anafahamu wazi atakutana na mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa.
Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo ,Anastazia Katunzi amesema morali ya wachezaji ipo juu na wanaufahamu umuhimu wa mchezo huo.
Katika kundi A, Mamelodi Sondowns Ladies wanaongoza wakiwa na alama sita, Jkt Queens ni ya pili na alama tatu huku Athletico Abidjan ikiwa na alama moja sawia na Sporting Casablanca.