Jkt Queens yatupwa kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika
IVORY COAST: Mabingwa wa soka la Wanawake nchini Jkt Queens wamepangwa kundi A katika michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa wanawake inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia novemba 5 –19, 2023 nchini Ivory Coast.
Mabingwa hao wa ukanda wa CECAFA wamepangwa kundi moja na timu za Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Athetico Fc Abidjan ya Ivory Coast na Sporting Casablanca ya Morocco.
Kundi B, lina Mabingwa watetezi wa michuano hiyo AS FAR ya Morocco, AS Mande kutoka Mali, Ampem Darkoa ya Ghana na Huracanes ya Equatorial Guinea.
Hii ni mara ya pili kwa timu kutoka Tanzania kushiriki michuano hiyo baada ya Simba Queens kushiriki msimu uliopita katika makala ya pili ya mitanange hiyo na sasa Jkt Queens wanakwenda kushiriki makala ya tatu ya michuano hiyo.