JKT yatangaza mafunzo ya kujitolea

JESHI la Kujenga Taifa(JKT) limetangaza nafasi za mafunzo ya JKT ya kujitolea kwa mwaka 2023.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Tawi la Utawala la JKT, Brigedia Jenerali Hassan Mabena alisema Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele amewaita vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwano wanaotaka kujiunga na mafunzo ya JKT ya kujitolea kwa mwaka 2023.

Alisema utaratibu wa kuomba na kuitwa unaratibiwa na Ofisi za wakuu wa Mkuu wa Mikoa na wilaya ambao mwombaji anaishi.

Aidha, Brigedia Jenerali Mabena alisema mwombaji mwenye sifa ya taaluma ya uhandisi wa ujenzi, ufungaji, umwagiliaji, uvuvi, saikolojia, na wanayamapori wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia mikoa yao.

Alisema, usajili wa vijana kujiunga na mafunzo ya jeshi la kujenga Taifa kwa kujitolea unatarajiwa kuanza agosti 28 mwaka huu kwa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Alisema, vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya jeshi la kujenga Taifa kuanzia Septemba 26 hadi 29 mwaka huu.

Aidha Brigedia Jenerali Mabena alisema Jeshi la Kujenga Taifa linapenda kuwa taarifa vijana watakaopata fursa hiyo kuwa haitoi ajira pia halihusiki kuwatafutia ajira katika asasi, vyombo vya ulinzi na usalama na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali bali hutoa mafunzo ambayo yatawasidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza mkataba wao na Jeshi la kujenga Taifa.

Aidha alitaja sifa za waombaji kuwa lazima awe raia wa Tanzania na kwa vijana wenye elimu ya darasa la saba wawe na umri wa miaka 16 hadi 18 na waliomaliza elimu ya msingi kuanzia mwaka 2020, 2021 na 2022 na awe na cheti cha kumaliza elimu ya msingi.
Alisema vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne wasiwe na umri wa zaidi miaka 20 na wawe wamemaliza masomo yao kati ya mwaka 2020 hadi 2022 na wawe na cheti halisi cha kumaliza Kidato Cha Nne na cheti halisi na awe na cheti halisi cha matokeo na akiwa amepata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la Nne.

“Kwa kijana aliyepata daraja la nne awe na ufaulu wa kuanzia 26 hadi 32.”

Kwa waliomaliza Kidato cha sita asiwe na umri usiozidi miaka 22 na awe amemaliza kati ya mwaka 2020 hadi 2022 awe na cheti halisi ya kumaliza masomo na cha matokeo na awe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la nne.
Alisema kwa waliomaliza elimu ya stashahada umri wao usizidi miaka 25, awe na chati cha Kidato cha Nne na cha chuo, huku walio na shahada asizidi miaka 26 wakati wenyewe shahada ya uzamili asiwe na umri usiozidi miaka 30.
“Pia awe na akili timamu, asiwe na a lama na michoro mawilini, na kutambulisho cha Taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button