JKT yatangaza nafasi za mafunzo yakujitolea

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limefungua rasmi usajili wa vijana kutoka Tanzania Bara na Visiwani kujiunga na Jeshi hilo kwa kujitolea.

Usaili wa nafasi za mwaka 2022, umeanza rasmi leo Agosti 25, kwa mujibu wa Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena.

Brigedia Jenerali Mabena amesema Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amewaalika vijana kutuma maombi kupitia ngazi za mikoa kote nchini.

Amesisitiza kuwa JKT haiajiri na kwamba nafasi hizo haziuzwi na hivyo watakaoomba wachukue tahadhali ya matapeli.

 

Habari Zifananazo

Back to top button