John Bocco aibukia JKT Tanzania

KLABU ya JKT Tanzania imetangaza kumsajili mkongwe John Bocco kwa ajili ya msimu wa 2024/25 kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Simba ilimkabidhi majukumu Bocco kuwa kocha mkuu wa kikosi cha Vijana wenye umri chini ya miaka 17 msimu wa 2023/24 ukielekea ukingoni.

“Hakuna muda wa kupoteza 💪 “TOP SCORER OF ALL TIME” ameshaanza mazoezi,”imesema taarifa JKT Tanzania kupitia ukurasa wa Instagram.

Soma zaidi:http://Bocco awapa somo wachezaji wenzake

Bocco mwenye umri wa miaka 34 alicheza Azam kuanzia 2007 akisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2014 kabla ya kuhamia Simba 2017.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button