Jokate atikisa mapokezi Mtwara
MTWARA; WANANCHI mkoani leo Mtwara wamejitokeza kwa wingi kumpokea Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Jokate Mwegelo, aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Abdi Mohamed Abdi.
Katibu Mkuu huyo yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja na atapata fursa ya kutembelea wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri kwenye Manispaa ya Mtwara Mikindani na maeneo mingine.
Akizungumza na kikundi cha Jitegemee, Jokate amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa kuwatafutia eneo wanakikundi hao litalowezesha kufanya shughuli zao hizo bila kubugudhiwa.
“Nikuombe mkurugenzi kuwatafutia eneo kikundi hiki cha vijana, ambalo watafanya kazi zao kwa uhuru bila kubugudhiwa,”amesema Jokate
Kikundi hicho kilianza na mtaji wa Sh milioni 10 kupitia mkopo wa halmshauri wa asilimia 10 lakini mpaka sasa wana mtaji wa Sh milioni 50.
Ziara hiyo atahitimisha kwa kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Mashujaa kwenye manispaa hiyo.