Jukwaa la kampeni laporomoka nchini Mexico laua watu tisa
Mexico City, MEXICO: BARAZA la Mawaziri la Mexico limesema kuwa jengo moja limeporomoka baada ya upepo mkali kuvuma katika mkutano wa kampeni ya mgombea urais Jorge Alvarez Maynez na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine 50 kujeruhiwa.
Mshuko huo ulitokea Jana wakati wa mkutano wa kampeni ya chama cha Citizens’ Movement katika Mji wa San Pedro Garza Garcia katika jimbo la Nuevo Leon. Video kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha jengo hilo likianguka mbele kwenye umati wa watu, na kuwafanya wahudhuriaji kukimbia hovyo.
Gavana wa Nuevo Leon Samuel Garcia alisema katika ukurasa wake wa X kwamba ametembea katika zahanati na hospitali saba na kutangaza kwamba waliofariki katika ajali hiyo ni watu wazima nane na mtoto mmoja na waliojeruhiwa ni wengi takribani 50.
Aliporudi mahali pa ajali hiyo baada ya kuondolewa katika hospitali ya eneo hilo, Alvarez Maynez, mgombea urais wa chama cha Citizens Movement, alisema anatarajia mamlaka zitachunguza kilichotokea huku akiomba uchunguzi huo uwe wa wazi ili kubaini chanzo halisi cha poromoko hilo.
“Sijawahi kuona kitu cha ghafla sana”, alisema Alvarez Maynez, akimaanisha jinsi upepo ulivyovuma ghafla na kusababisha maafa hayo.
Wajumbe wa walinzi wa kitaifa wa Mexico na jeshi walikuwa mahali hapo kutoa msaada, waziri wa mambo ya ndani Luisa Alcalde alisema kwenye mitandao ya kijamii wakiwataka wananchi wao wawe na utulivu wakati serikali inajaribu kuweka sawa hali hiyo.
Matukio ya kampeni yanafanyika wiki hii ambapo Juni 2 kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Majimbo na Manispaa nchini humo.
Alvarez Maynez, ambaye sasa amesimamisha hafla za kampeni, yuko katika nafasi ya tatu katika uchaguzi, akimfuata Claudia Sheinbaum wa chama tawala cha Morena na mgombea wa muungano wa upinzani Xóchitl Gálvez.
Kampeni hiyo hadi sasa imekumbwa na mauaji ya takriban wagombea wa ofisi za mitaa ishirini.