JUKWAA la Mitindo la kuonyesha mavazi nchini Tanzania Lady in Red limekuja kivingine ni usiku wa kuonesha mavazi yatakayo saidia watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete.
Onyesho hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii February 17 katika ukumbi wa Were house uliopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Habari leo Mwandaaji wa jukwaa la Lady in Red, Kampuni ya Hudo Domingo, Mary Fernandes amesema kuwa wamefanya mchujo wa wanamitindo (model Casting) walikuwa zaidi ya 200 wamepatikana 23 watakaopanda kwenye jukwaa hilo.
“Kama kawaida yetu kila mwaka tunaangalia wapi tukapeleke kusaidia wenye uhitaji, mwaka huu tumelenga kuwasaidia watoto wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete waliopata matibabu na bado hawajalipia tutawalipia.”amesema Mary
Amesema gharama za matibatu ni kuanzia laki nane na kuendelea hivyo kwenye onyesho hilo wataingia na kiingilio VIP 50000 na kawaida elfu 30000 kitakachosaidia kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo.