WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso anatarajia kuzindua kongamano la pili la Kimataifa la Sayansi ya Maji linalotarajia kufanyika siku tatu jijini Dar es salaam.
Akizungumza mkuu wa chuo cha maji , Adam Karia alisema kongamano hilo litaanza Mach 8 hadi Mach 11 mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza.
Alisema zaidi ya mataifa 12 yanatarajia kufika katika kongamano hilo ili kuonesha vifaa vyao na utendaji kazi, lakini pia zaidi ya dondoo ya mijadala 70 yanatarajiwa kufikishwa na wataalam mbalimbali kutoka nchi tofauti kwa njia ya moja kwa moja na wengine kwa njia ya mtandao wa mubashara (zoom) kwajili ya kujadiliana.
“Ni kongamano linalokusanya watu kutoka idara zote, lakini pia tunapokea watu wa aina zote, wakiwa watu wa kawaida na watu wa kwenye taasisi au shuleni na vyuoni ili waje kujifunza.”alisema Karia.
Lakini pia tunaruhusu hata wanafunzi kutoka katika shule mbalimbali na vyuo tofauti kuudhulia kongamano hilo kwaajili ya kujifunza” alisema Karia.
Alisema watu wa taasisi zingine pia wanahitajika kufika kongamano hilo kwakuwa wao ndo watumiaji wakubwa wa maji safi hivyo wanaweza kupata elimu na kutumia maji mengine mbadala na kuyaacha hayo ambayo yanahitajika na watu wengi kwaajili ya matumizi ya nyumbani.
Alimalizia kwa kusema kufanyika kwa kongamano hili la pili kunatokana na mafanikio ya kongamano la kwanza lililofanyika mwaka jana katika ukumbi wa kimataifa Mwalimu Nyerere mkoani Dar es salaa.
Lakini pia alisema kutakuwa na maonesho mbalimbali kutoka katika taasisi zingine za maji hivyo ni muda mzuri kwa watu na taasisi kuja kujigunza masuala ya maji.