Klabu ya Juventus ya nchini Italia imekatwa pointi 15 za Seria A huku baadhi ya viongozi wake akifungiwa kutokana na kukiuka kanuni za mauzo na manunuzi ambapo kuna udanganyifu wa bei juu ya uhalisia wa kununua na kuuza wachezaji ambapo mamlaka nchini Italia zimebaini.
Miongoni mwa waliofungiwa ni aliyekuwa Rais, Andrea Agnelli ambaye amefungiwa miaka miwili huku Mkurugenzi wa Tottenham ambaye aliwahi kuhudumu Juventus amepewa kifungo cha miaka miwili na nusu nje ya soka.
Kwa mujibu wa Skysport, Mkurugenzi wa Mashtaka wa FIGC, Giussepe Chine awali alipendekeza Juventus kupokonywa pointi tisa na endapo wakikata rufaa na kukataliwa wakatwe 15, lakini Shirikisho limechukua uamuzi tofauti na Juventus wamenyang’anywa pointi 15 na sasa wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo.
Marufuku ya miaka miwili na nusu kwa mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Juventus, Fabio Paratici ambaye sasa ni mkurugenzi mkuu wa soka Tottenham Spurs, inajumuisha ombi la kuongezewa muda ili kugharamia shughuli za Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA).