Jux asogeza mbele uzindua wa albamu

MSANII nyota wa muziki nchini, Juma Mussa maarufu kama ‘Jux’ ametangaza kusogeza mbele uzinduzi wa albumu yake mpya ‘King Of Hearts’ ambapo uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Disemba 7 mwaka huu katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Jux ameeleza kwamba amefanya maamuzi hayo ili kuhakikisha wasanii wote walioshiriki kwenye album yake wana perform siku ya uzinduzi ndani ya ‘The Super Dome’ Masaki.

Amesema siku ya uzinduzi kutakuwa na surprise kibao na kuweka historia ya kipekee katika albamu yake.

“Siku ya tarehe 7 Disemba nataka iwe siku ya Industry nzima kuweka historia.

Kuanzia ukumbi ambao itafanyika Show hii, Stage, Mavazi, Performance na kila kitu ” – ameeleza

Habari Zifananazo

Back to top button