Jwaneng hawana presha

WAKATI Simba SC wakijiandaa na mchezo wa mwisho kundi B kesho huku kauli mbiu yao ikiwa ‘Vita ya Kikasi’ wapinzania wao Jwaneng Galaxy ni kama hawatishiki na vita hiyo.

Simba inahitaji ushindi wowote kwenda hatua ya robo fainali, kama atatoa sare au kufungwa na Wydad kushinda dhidi ya Asec Mimosas rasmi Simba ataondoshwa kwenye michuano hiyo.

Akizungumzia mchezo huo, kocha wa Jwaneng, Morena Ramoreboli amesema lengo lao sio kuingia kwenye kisasi hicho bali shabaha yao ya kwanza kushinda mchezo huo.

Advertisement

“Hatuko hapa kucheza kisasi na Simba, walipoteza 5-0 dhidi ya Yanga SC na wakati mwingine nao pia waliitawala Yanga kwahiyo ndivyo ulivyo mpira wa miguu,”amesema kocha huyo.