TUME ya TEHAMA imezindua rasmi kongamano la saba la TEHAMA litakalofanyika Dar es Salaam kuanzia Oktoba 16 hadi 20, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine wataalamu hao watajadili maendeleo ya akili mnemba ‘artificial intelligence’.
–
“Tutajadili kuhusu teknolojia zinazo chipukia. Miongoni mwa teknolojia hizo ni pamoja na Akili Mnemba kwa ajili ya kutengeneza kazi kwa vijana na kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dk. Nkundwe Mwasaga.
–
Kongamano hilo la saba ni kiungo kikubwa kinachowaunganisha wawekezaji, wabunifu, wataalam, waajiri, vijana, nakadharika. Dk Mwasaga pia amezindua pia Kadi maalum kwa ajili a wataalam wa TEHAMA na washiriki wa kongamano la mwaka la TEHAMA.
Kadi hiyo yenye microchip inauwezo wa kumtambukisha mtaalama aliyesajiriwa na TUME ya TEHAMA na pia washiriki wote wa kongamano hilo wa ndani na nje ya nchi.