Kagame ataka historia ya Rwanda ihifadhiwe

RAIS Paul Kagame amewataka wataalamu wa historia na watafiti wa masuala ya historia kushirikiana ili kutengeneza historia ya Rwanda kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo kujua ilipotoka Rwanda, ilipo na inapoelekea.

Alitoa mwito huo kupitia ujumbe mfupi uliorekodiwa katika mfumo wa video na kurushwa katika mitandao ya kijamii ya vyombo vya habari vya taifa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Utafiti Kuhusu Mauaji ya Kimbari ya 1994, kwa ajili ya kuwafikia wananchi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kongamano hilo lililokuwa na kaulimbiu isemayo: “Ujuzi, Chanzo na Rasilimali Wakati wa Maangamizi ya Watutsi” liliandaliwa na Wizara ya Umoja wa Kitaifa na Ushiriki wa Kiraia (MINUBUMWE) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Rwanda na Mwanahistoria wa Ufaransa, Vincent Duclert.

“Mfanye kazi vizuri kwa uhuru kwa kutumia vyanzo na mbinu mbalimbali mkiongozwa na Profesa Vincent Duclert ingawa ripoti zenu haziwezi kuwa za mwisho katika utafiti,” alisema Rais Kagame.

 

Habari Zifananazo

Back to top button