Kagame autaka tena urais

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amesema atawania muhula wa nne katika uchaguzi wa rais mwaka ujao.
–
“Ndiyo, hakika mimi ni mgombea,” Kagame aliambia jarida la Kifaransa Jeune Afrique Jana.
–
Alipoulizwa kuhusu mataifa ya Magharibi yangefikiria nini kuhusu uamuzi wake wa kugombea tena, Kagame alisema, “Pole kwa nchi za Magharibi, lakini kile ambacho nchi za Magharibi hufikiri sio tatizo langu.
–
“Nimefurahishwa na imani ambayo Wanyarwanda wanayo kwangu. Nitawatumikia daima, kadri niwezavyo.”aliongeza.